Thursday, May 9, 2024
spot_img
HomeKiswahili newsMagoha alitangazia wenzake tutaoana baada ya kunijua kwa siku tatu pekee, asema...

Magoha alitangazia wenzake tutaoana baada ya kunijua kwa siku tatu pekee, asema Mjane

Na Iptisam Abdallah

Ibaada ya wafu ya aliyekuwa Waziri wa Elimu George Magoha imefanyika leo huku familia , marafiki na maafisa wa ngazi za juu serikalini wakihudhuria hafla hiyo.

Ibaada ya wafu ya mwenda zake ilifanyiwa  Kanisa Katoliki  la  Consolata jijini Nairobi.

Magoha aliifariki dunia mnamo Januari 24, mwaka huu nyumbani kwake Nairobi  akiwaacha nyuma mjane Barbara Odudu na mwanawe wa pekee Michael Magoha.

Akisherehekea maisha ya mumewe , Dkt. Barbara asema kuwa hayati alikuwa mtu mwenye maono na ari ya mafanikio.

George Magoha

‘’Maisha ya Prof. George Magoha yalijengeka katika nguzo tatu muhimu akiwemo Mungu aliyemwabudu, Shule ya upili ya Starehe iliyomfinyanga na kuwa mtu mwadilifu na Taaluma ya utabibu iliyoyazunguka maisha yake yote,” Barbara aliwaambia waombolezaji

Akiizungumzia safari yake ya ndoa na hayati mumewe, Dkt. Barbara alisema kuwa ilikuwa ya kuthaminika. “ Nilikutana na Prof. George Magoha mjini Lagos nchini Nigeria mwaka wa 1972 alpokuja kusomea udaktari kupitia ufadhili aliopewa. Baada ya miezi miwili, alianza kuwaambia watu kuwa anataka kunioa,”

Akasema : “ Nilimweleza mamangu kuwa nilitaka kuolewa naye na akanisihi ningoje afunge na kuomba kwa siku tatu mtawalia ili Mungu amwonyeshe ikiwa mwanamume huyo alinifaa. Baada ya siku tatu, mama alionyeshwa ndotoni kuwa Prof. Magoha angekuwa na mafanikio mengi maishani na kudura ilitaka tuungane,”

Barbara alisema kwamba mamake mzazi  alimruhusu kuolewa na Magoha iwapo tu iwapo angekuwa na subira amalize masomo yake ya udakitari.“Mume wangu alitimiza masharti haya na tukaoana. Alimhudumia mamangu mpaka mwisho wa maisha yake mnamo 2008,”

Alisema kwamba siku ya kifo chake, alikuwa anapiga pasi ili aelekee kazini .

“Aliniambia hakujisikia vizuri nikamshauri ajipumzishe. Ghafla , alipatwa na mshtuko wa moyo uliojirudia mara tatu. Niliyakumbuka maneno yake aliposema kuvile wa lolote litakapompata nimwite Prof.Omwanda. Nilimpigia simu, akafika na kumpima presha. Vilevile nilimpigia mwanangu Dkt. Michael Magoha simu aje haraka,” Barbara alisema

“ Mume wangu alizungumza na mwanawe kabla ya kuoatwa na mshtuko wan nne na kisha kuiaga dunia.’’ Aliongeza Dkt. Barbara Odudu huku akiyazuia machozi yasimtiririke.

Prof George Magoha

Prof Magoha alizaliwa mnamo Julai 2, 1952 mjini Kisumu, alikuwa msomi mashuhuri, daktari wa upasuaji, Mwenyekiti wa Baraza la Mitihani nchini (Knec) na baadaye Waziri wa Elimu.

Alikuwa mtu mwenye tambo kakamavu na aliyechukia ufisadi. Elimu yake ilianzia katika Shule ya Msingi ya  Dr. David Livingstone Nairobi na baada ya kuhitimu akajiunga na Shule ya Upili ya Starehe Boys Centre and School.

Magoha alifuzu na diploma ya masomo ya A levels katika chuo cha Strathmore School na kupata ufadhili wa kusomea udaktari katika Chuo Kikuu cha Lagos nchini Nigeria.

Elimu yake ya udaktari ilimfikisha Lagos University Teaching Hospital na  the University College  Hospital nchini Nigeria.

Vilevile, alifanikiwa kwenda the Royal College of Surgeons Ireland, Royal Postgraduate Medical School na  Hammersmith Hospital London. Katika hospitali hizo aliukuza ujuzi wake katika utabibu.

Katika Nyanja ya kazi, Prof. George Magoha alikuwa mhadhiri katika kitengo cha elimu ya upasuaji katika Lagos University Teaching Hospital.

Mnamo 1988, alijiunga na Chuo Kikuu cha Nairobi na kuhudumu kama mhadhiri katika kitengo cha upasuaji wa urolojia na kuoanda daraja na kuwa profesa kamili wa upasuaji mnamo 2000.

Aidha, alihudumu katika nyadhifa mbalimbali Katika chuo kikuu cha Nairobi akipanda kutoka mwenyekiti wa idara hadi kuwa makamo Chansela mnamo Januari 2005.

Mazishi ya hayati Prof. George Magoha yameratibiwa kufanyika Februari 11 nyumbani kwake Umiru ndani ya  Nyamninia huko Yala .

Katika taarifa zilizotolewa kwa vyombo vya habari, Julius Jwan, Msemaji wa Kamati ya Familia na Mipango ya Mazishi alisema kuwa misa ya mazishi itafanyika Februari 11  ndani ya Chuo Kikuu cha  Odera Akang’o University Campus Yala.

Mwisho

 

 

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
Google search engine

Most Popular

Recent Comments

Rodgers Wakhisi on Buriani Walibora