Thursday, May 9, 2024
spot_img
HomeKiswahili newsKiswahili Kipigwe Jeki

Kiswahili Kipigwe Jeki

Na Irene Nasimiyu

Kiswahili ni lugha ambayo inatuweka pamoja kama Taifa. Katika uzungumzaji,  lugha inayoeleweka hutumika ili ujumbe uweze kueleweka. Hivyo basi Kiswahili ni Lugha ya Taifa. Chambilecho wanalugha Kiswahili Kitukuzwe kwani lugha ya taifa!

Lugha ya Kiswahili hutumika katika hafla mbalimbali nchini. Kwa mfano wanafunzi huzungumza Kiswahili siku ya Ijumaa katika shule zao. Iwapo mwanafunzi atapatikana akizungumza lugha nyingine basi huenda akapata adhabu.

Sheria ambazo huwekwa katika kuzungumza lugha hii shuleni ni kuhakikisha kuwa mwanafunzi anafuata ngeli sahihi katika kutunga sentensi zake, mwanafunzi vilevile lazima aelewe aina za maneno amabazo hutumika katika kufanikisha sentensi kwa mfano nomino,kitenzi,viwakilishi na kadhalika.

Irene Nasimiyu

Kiswahili kwa upande mwingine ni lugha ambayo imedhalilishwa sana. Mara nyingi utawasikia wahutubu wakizungumza kimombo tu huku wakidai kuwa lugha ya Kiswahili ni ngumu na isiyohitaji wasomi. Katika shule, walimu wametilia mkazo lugha nyingine na kuwaachia walimu wa Kiswahili kupambana na wanafunzi hasa wakati wa matumizi ya luha hii.

Ni bora kuwaelimisha wanajamii kwa jumla kuwa Kiswahili kinalipa. Kwa mfano katika kuandika vitabu vya Kiswahili,kuandaa vipindi vya Kiswahili,kufunza Kiswahili katika vyuo vikuu vikuu na hata katika kuwa mhutubu bora wa Kiswahili.

Nilipokuwa katika shule ya sekondari niliandika makala mazuri katika gazeti la Taifa leo.Makala hayo yaliinua hadhi ya shule hiyo hadi mwalimu mkuu wakati ule Bi Petronillah Lumbasi akanitunuku safari ya kuelekea Thomsons Falls ili nifurahie mandhari ya huko.

Hii ni zawadi ambayo huenda singepata iwapo singeandika makala haya. Wadau! Kiswahili kinalipa. Huenda safari ikawa ni ndefu lakini utakapoanza kuvuna matunda basi utafurahia matunda ya Kiswahili.

Mwisho

 

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
Google search engine

Most Popular

Recent Comments

Rodgers Wakhisi on Buriani Walibora