Saturday, April 20, 2024
spot_img
HomeKiswahili newsMama Ngina amfokea Ruto kwa madai ya kukwepa kulipa ushuru

Mama Ngina amfokea Ruto kwa madai ya kukwepa kulipa ushuru

 

Na Dante Kayugira, Nairobi

Aliyekuwa mke wa Rais Mzee Jomo Kenyatta, Mama Ngina amejitokeza kwa mara ya kwanza kutetea madai ya kwamba familia yake imekuwa ikikwepa ushuru kwa muda mrefu.

Mama Ngina, ambaye alizungumza katika Kanisa ya Katoliki la Mtakatifu Teresa huko Mpeketoni, Kaunti ya Lamu, alisema yuko tayari kupigwa mnada kwa uthibitisho wa Serikali kukwepa kulipa kodi.

“Ni ukweli kwamba kila Mkenya aliyeajiriwa anapaswa kulipa kodi ya mapato, bila kujali kundi lao la kazi.  Hilo halifai kuwa majadiliano.  Hakuna haja ya kumtukana mtu, kuonekana kana kwamba unafanya jambo fulani,“ Mama Ngina alisema

Akaongezea : “Kodi ni lazima Kwa Kila mtu kulingana na uwezo wako na SI jambo la kuzungumzia Kila mahali kwenye vyombo vya habari.“ Ukikosa kulipa Kodi unapelekwa kortini. Ukikosa kulipa Kodi vitu zako zitachukuliwa Ili kulipa kodi. Haifai kumharibia mtu yeyote jina. Mtu anafaa kushtakiwa Ili alipe kile anachofaa kulipa.”

Hii ni baada ya Rais William Ruto na viongozi wa mrengo wa Kenya Kwanza kutaka familia hiyo ilipie ushuru wa mali yote wanayomiliki.

Viongozi hao waliweka wazi kuwa Kuna milioni 350 wa msamaha wa Kodi uliopewa benki za NCBA na NIC.

Aliyekuwa Katibu wa Hazina Kuu ya Serikali, Henry Rotich hakutoza  hisa za CBA Kwa NIC Kwa kulipa ushuru wa stempu ya asilimia moja ya thamani ya hisa ambazo hazijanukuliwa zinazohamishwa.

Mwisho

 

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
Google search engine

Most Popular

Recent Comments

Rodgers Wakhisi on Buriani Walibora