Friday, March 29, 2024
spot_img
HomeUncategorizedMwanamke achomwa na maji moto na mumewe mjini Kakamega

Mwanamke achomwa na maji moto na mumewe mjini Kakamega

Seliphar Musungu

 Mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 23 anauguza majeraha mabaya ya moto na ya  kupigwa mwilini mwake  katika mtaa wa  Mulunyu  mjini Kakamega.

Gentrix Kahela Njoroge alichomwa na maji moto  na kupigwa kitutu na mumewe wa miezi saba. Unyama huo ukimwacha Gentirx na vidonda vikubwa.

 Alielezea kwamba chanzo cha haya yote ni baada ya kuamua kukatisha uhusiano wake na mumewe baada ya kugundua kwamba mumeweana mke mwingine. 

“Niliamua kuondoka kurudi nyumbani baada ya kwenda muda mchache alinifuata kwa pikipiki na kuanza  kunipiga njiani baadaye akanirudisha kwa nyumba aliponitendea unyama huu.” Gentrix aeleza.

Gentrix alisema kwamba baada ya kupigwa na kuchomwa mumewe alimfungia chumbani hata asipate nafasi ya kwenda haja.

Gentrix hakupata matibabu yoyote na baada ya wiki moja mumewe alimsafirisha hadi kapenguria anakokaa dadake likini dadake alikataa na gentrix kurudishwa kakamega.

“Baada ya wiki moja alinipeleka kwa dadake kapenguria lakini dadake alikataa akihofia kwamba nangefariki wakati wowote kutokana na hali yangu. Alinirudisha nyumbani nilipomwambia kwamba nataka kurudi kwetu alisema kwamba ataleta dakitari anipe matibbau ya nyumbani.”   Gentrix asema

Familia yake Gentirx imeghadhabishwa na  kitendo hicho na kuomba serikali kuingilia kati ili mshukiwa huyo aweze kutiwa mbaroni.

Kulingana na nyanya yake gentrix hii sio mara ya kwanza mumewe Gentrix amemtendea mnyama huo. Anasema kwamba mwaka jana  mumewe Gentrix alimpiga na  akarejea nyumbani. 

“Tangu mwaka uliopita mwezi wa nane alipoondoka hapa nyumbani sisi kama familia tunamuona leo tena kama amejeruhiwa vibaya zaidi ukilinganisha na mara ya kwanza.”  Nyanya yake Gentrix asimulia

Mama yake kwa upande mwingine anadokeza kuwa uhusiano wa mwanawe na mumewe haujakuwa wa manufaa kwa manawe maana amekuwa akidhulimiwa na kuumizwa sana.  Mamake pia alieleza kwamba tangu mwanawe arudishwe nyumbani hajapata matibabu maana hawana pesa za matibabu. 

Familia hiyo inaomba serikali kufanya uchunguzi ili wanao tenda unyama huu waweze kutiwa mbaroni na kufunguliwa mashtaka ili kuwanusuru wale wote wanaopitia hali ya unyanyasaji wa aina hii.

Mwisho

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
Google search engine

Most Popular

Recent Comments

Rodgers Wakhisi on Buriani Walibora