Tuesday, April 16, 2024
spot_img
HomeUncategorizedWatu wanaoishi na ulemavu wafaidika na msaada wa vyakula Bungoma

Watu wanaoishi na ulemavu wafaidika na msaada wa vyakula Bungoma

Bungoma

Na Tony Wafula

Zaidi ya walemavu 100 wamenufaika na msaada wa vyakula kutoka kwa wanafanyabiashara katika kaunti ya Bungoma almaarufu Chamber of Commerce.

Msaada huo unapania kuwaokoa wengi wao kuangamia kutokana na makali ya njaa ambayo inaendelea kutikisa ulimwengu wote kufuatia virusi vya korona.

Kufuatia angizo la serikali kwamba hakuna kutangamana katika vukundi, wengi wa wakenya wanafanya kazi yao wakiwa manyumbani mwao na wale wa vibarua vya kila uchao wakiendelea kuumia.

Wengi wa walemavu katika kaunti ya Bungoma walikuwa wamesaulika na kaunti hiyo.

Akizungumza wakati wa kupeana vyakula hivyo Bwana John Wafula mwenyekiti wa Chamber of Commerce Bungoma alisema kuwa walemavu wengi walikuwa wamesaulika katika jamii na huu ndio wakati wahisani inafaa wajitokeze ili waweze kusaidiwa.

‘’Leo tunapeana vyakula kwa walemavu 100, ambapo wengi wao hawana mapato ya kila siku na pia hawana wakutegemea katika Maisha yao.’’ Alisema Wafula.

Alisema kuwa Kaunti ya Bungoma yafaa iliorodheshwe kwa kaunti ambazo ziko katika hatari ya mafuriko, akiongeza kuwa Watapeana msaada wa vyakula katika maeneo ya Dorofu, Bumula, Cheptais,Siloba.

Wakati huo huo Bwana Wafula alisema kuwa muungano wa wanabiashara hao unalenga kusaidia vijana ambao hawana ajira katika kaunti ya Bungoma hivi karibuni.

‘’Tunajua huu ni wakati mugumu kawa vijana wetu, wengi wao walikuwa wanafanya kazi za sulubu ili kupata chakula cha siku,’’ alisema.

‘’Tumefikia maeneo kadhaa ya mafuriko katika kaunti hii, wale waadhiriwa wa Cheptais tulikuwa huko tukawapa msaada na pia tunashukuru zile shule ambazo zimepeana msaada wa malazi.’’ Alisema

Ronald Siundu Wafula kutoka wadi ya Bukembe Magharibi, eneo Bunge la Kanduyi mmoja wa walionufaika na msaada huo alisema kuwa wengi wa walemavu walikuwa wamesaulika katika jamii akipongeza ushikiano wa wanabiashara hao na serikali ya Gavana Wycliffe Wangamati.

‘’Leo ni siku kubwa sana kwetu, Wanabiashara wa kaunti hii pamoja na uongozi wa kaunti kwa kutubariki na vyakula ambavyo vitatusaidia takribani mwezi mmoja.’’ Alisema.

Kwingineko katika Wadi ya Bukembe Magharibi eneo bunge la kaunti kaunti ya Bungoma wahisani walipeana vyakula kwa wajane wapatao 70.

Wakiongozwa na George Barasa msaidizi katika afisi ya Waziri wa barabara katika kaunti ya Bungoma, Timothy Wekesa Mwanahabari wa Kituo cha Sema Fm Webuye na Mercy Ngoya wa kituo cha Emuria Fm Busia walipeana Vyakula,sabuni na barakoa ambavyo vitasaidia wajane hao wakati huu mugumu.

George Barasa alisema kuwa ataendelea kusaidia wajane hao wakati huu mugumu wa korona virus na kuwaomba wahisani wengine kujitokeza na kusaidia watu wasiojiweza katika jamii zetu.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
Google search engine

Most Popular

Recent Comments

Rodgers Wakhisi on Buriani Walibora